Home Habari za michezo KISA USAJILI WA RONALDO…AL-NASSR YAMFUKUZA MCHEZAJI MWEUSI…

KISA USAJILI WA RONALDO…AL-NASSR YAMFUKUZA MCHEZAJI MWEUSI…

Ronaldo and Vincent

Klabu ya Al-Nassr inayoshiriki Ligi Kuu ya Saudi Arabia imekatiza mkataba wa mshambuliaji wa Cameroon Vincent Aboubakar ili kumpisha straika mpya Cristiano Ronaldo.

Kwa mujibu wa kanuni za ligi hiyo, klabu zinaruhusiwa tu kuwa na wachezaji wanane wasio raia wa Saudi Arabia.

Kabla ya ujio wa Ronaldo, Al-Nassr ilikuwa imefikisha idadi ya wachezaji wanaoruhusiwa kwa hivyo ilikuwa lazima mmoja wao angetimuliwa ili kutengeneza nafasi ya nyota huyo wa Ureno.

SOMA NA HII  SAFARI YA KAMBI MAREKANI YAZIDI KUNUKIA YANGA....GSM AGOMA KURUDIA YA MOROCCO MWAKA JANA...