Mtanzania wa kwanza kumiliki klabu Uingereza
Habari za michezo

HUYU HAPA MTZ WA KWANZA KUMILIKI KLABU UINGEREZA…ALISEPA BONGO AKIWA ‘YANKI’ TU…

admin January 10, 2023 9:32 pm

Klabu ya Oxford United iliyocheza na Arsenal na kupokea kichapo cha 3-0 kwenye kombe la FA imewahi kumilikiwa na Mfanyabiashara Firoz Kassam (68), mwenye asili ya India aliyezaliwa na kukulia Tanzania.

Akiwa na umri wa miaka 19 Kassam aliondoka Tanzania akaenda Uingereza kabla ya kuinunua klabu hiyo mnamo 1999 na kudumu nayo mpaka alipoiuza mnamo 2006.

Mwaka 2009 Kassam alitajwa kwenye Gazeti la The Times kama Mtu wa 309 kwa utajiri Uingereza akiwa na utajiri wa Pauni milioni 180.

Mnamo 2007, thamani yake ya jumla ilikadiriwa kuwa pauni milioni 240. Miaka 10 baadae thamani yake ilipanda mpaka pauni milioni 315 akitajwa kwenye orodha ya Matajiri ya Sunday Times ya 2017.

SABILO WA MBEYA CITY KUIBUKIA SIMBA SC….ATULIZA PRESHA….JAMBO LITAKUWA HIVI… SAKATA LA FEI TOTO…NABI AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA…VIGINGI 6 VYA MRAZILI SIMBA HIVI HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply