Habari za Yanga
Habari za michezo

LILE DILI LA BEKI KITASA KUTUA YANGA ..UKWELI UKO HIVI…JAMAA NI BEKI KWELI KWELI….

admin January 11, 2023 12:35 pm

Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa itafanya usajili wa wachezaji wawili kabla ya kufungwa kwa Dirisha Dogo la Usajili, Januari 16.

Yanga imekua ikisubiriwa kwa hamu kufanya usajili huo, baada ya kuhusishwa na majina kadhaa ya wachezaji ambao wamewahi kuwika na klabu za Soka nchini Tanzania na nje ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino wa Klabu hiyo inayoshikilia Taji la Tanzania Bara Ally Kamwe amesema, wamepanga kusajili Wachezaji wawili wa Kimataifa wa Kigeni wanaocheza nafasi za Ushambuliaji wa Kati na Beki wa Kati.

Ally Kamwe amesema katika eneo la Beki watasajili Mchezaji ambaye anashiriki kwenye Michuano ya Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN’ Mwezi huu ingawa hajamueka wazi.

Pia Ally Kamwe amekanusha Tetesi za Klabu hiyo kumuwinda Mshambuliaji wa zamani wa Wydad Casablanca Francy Kazadi, ambaye kwa sasa anawika na kikosi cha Singida Big Stars FC, katika Michuano ya Kombe la Mapinduzi 2023 inayoendelea Kisiwani Unguja ‘Zanzibar’.

KISA KUWA WANIGERIA…OKWA NA AKPAN WAACHWA NA SIMBA…ISHU NZIMA IKO HIVI… KUHUSU ISHU YA USAJILI SIMBA NA DILI LA MANZOKI…KAULI YA MO DEWJI HII HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply