Mwakinyo na Manara
Burudani

KISA KUACHANA NA MKEWE…MWAKINYO ALIPIZA KISASI…AMPIGA KIJEMBE KIZITO MANARA…

admin January 12, 2023 6:58 am

Bondia mkubwa Bongo, Hassan Mwakinyo amemshushia dongo zito Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara baada ya kuachana na mkewe mdogo ambaye alifunga naye ndoa hivi karibuni huku chanzo kikidaiwa kuwa ni ugomvi kati ya wanandoa hao.

Bondia huyo kupitia mitandao yake ya kijamii amemponda Manara na kumsihi aache kuoa hovyo kwa kile alichodai kuwa hata Mtume amesema hivyo.

“Kuoa mke zaidi ya mmoja yataka kifua jaman msioe watoto wa dogo kama hamviwezi msione fasheni kujiolealea ovyo ovyo tu, sababu hawafuati kula hao watoto wa watu baadae inakuwa hidhara yani!! inshot usioe kama huviwezi Mtume mwenyewe kasema,” ameandika Mwakinyo.

Ikumbukwe pia kuwa, mnamo mwezi Septemba 2022 baada ya Mwakinyo kupigwa huko London, Manara alikuwa mtu wa kwanza kumshutumu bondia huyo kuwa ameuza pambano hilo licha ya Mwakinyo kukana na kudai kuwa aliumizwa na viatu.

Mengi yalizungumzwa na Manara, ugomvi ukawa mkubwa lakini hakuna ambaye anajua wawili hawa walimaliza tofauti zao au hawakumaliza.

Ujumbe wa Mwakinyo leo hii ni uthibitisho tosha kwamba yeye na Manara bado hawajamaliza tofauti zao.

SIMBA WAMTUMIA STRAIKA MKATABA…MBRAZILI AMTAJA…YACOUBA OUT YANGA….KISINDA MSALA TUPU… YA FEI TOTO YANUKIA SIMBA…MKWANJA ANAOKUNJA PETER BANDA NI KUFRU TUPU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply