Habari za Yanga
Habari za michezo

KISA KURUDISHWA YANGA NA TFF…RAGE AIBUKA NA ‘NONDO HIZI MPYA’ KWA FEI TOTO…

admin January 12, 2023 8:12 pm

Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Ismail Aden amemuonya mchezaji Feisal Salum Fei Toto akikata rufaa Mahakama ya usuluhishi ya FIFA (CAS) atakuwa anapoteza muda tu.

Badala yake, Rage amemtaka Fei Toto akae chini tu na Yanga na awe mpole badala ya hiki anachojaribu kukimbilia CAS kwani maamuzi ya Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji kuwa yeye ni mchezaji halali wa Yanga hayawezi kutenguliwa huko.

“Unapotaka kufungua kesi CAS kwanza uwe na hakika sheria za FIFA zimevunjwa, sasa hili la Fei hakuna sheria za FIFA zilizovunjwa bali sheria zilizovunjwa ni za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Huko atapoteza muda na anaweza kuadhibiwa zaidi maana kwanza kabla ya kufungua kesi unatakiwa uweke kama dola Elfu 10 (Sh Milioni 23 za Tanzania) tena hiyo uwe na uhakika kama utashinda, ukishindwa adhabu yake inaweza kuwa kubwa kwake Fei, hivyo awe makini na wale wanaomshauri,” amesema Rage.

MPANGO WA SAMATTA KURUDI KUKIPIGA LIGI YA BONGO WAIVA…AITAJA SIMBA… SIMBA WAFUATA MASTAA WAWILI UARABUNI…KIKOSI CHA FUMULIWA CHOTEE…YANGA WATUA CHAN…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply