Habari za Yanga
Habari za michezo

SAKATA LA FEI TOTO NA YANGA….KWA MARA YA KWANZA SENZO AFUNGUKA MCHEZO ULIVYO…AITAJA CAS…

admin January 15, 2023 12:51 pm

Senzo Mbatta aliyekuwa CEO wa Simba SC na Yanga SC kwa nyakati tofauti, amesema kesi ya Feisal Salum kama ataenda CAS itakuwa ngumu kwake kwa babu kuna vitu vingi amekosea.

Senzo amesema; “Maombi ya Feisal Kuvunja mkataba na yeye kwenda kuilipa Yanga kabla ya kutuma maombi ya kuvunja huo mkataba na kuanisha sababu za kutaka kuvunja mkataba.

“Muda wa kuvunja mkataba haukuwa sahihi huwezi kufanya jambo kama hili katikati ya msimu bila sababu maalumu maana sheria zipo wazi zinasema lazima uainishe vifungu vilivyokiukwa kwenye mkataba wako ndio uvunje mkataba.

“Timu iliyomtaka ilipaswa lazima iandike barua Yanga kabla ya kulipa release clause ya kiasi kilichoanishwa.

“Iwapo imetokea bahati imewezekana Feisal Salum anavunja mkataba , Sheria za FIFA zimesema itawezekana siku 15 kabla ya mwisho wa msimu kama kutakuwa na mazingira magumu kwake [Difficult Case].”

Senzo amemaliza kwa kusema Kwa maana hiyo FEITOTO ana makosa mengi amefanya, ila FIFA Hawawezi kumfungia ila watamuambia arudi klabuni acheze.

KUHUSU MBRAZILI SIMBA KUMKUBALI GHAFLA….MINZIRO AANIKA ‘UCHAWI’ ANAOTUMIA KIBU DENIS.. HAZIRA ZA SOPU ZAHAMIA KWA MANULA WA SIMBA…DENI LAKE LAZIDI KUKUA KILA SIKU….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply