Habari za Simba
Habari za michezo

MZEE DALALI ATAKA WANAOWANIA UBOSI SIMBA WAFUNGUKE WATAKAVYOIFUNGA YANGA TU…

admin January 17, 2023 6:13 pm

Yanga imetajwa kwenye ufunguzi wa kampeni za wagombea wa uongozi wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa Simba, ikipigiwa mahesabu namna ya kushushwa kileleni.

Kampeni hizo zimefunguliwa rasmi jana na zitafanyika kwa siku 12 ambapo uchaguzi utafanyika Januari 29 mwaka huu.

Ipo hivi, aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Hassan Dalali amewataka wajumbe kuwauliza maswali wagombea kwamba watafanya nini ili Simba iweze kuchukua ubingwa msimu huu pia kuifunga Yanga katika mechi yao ya mzunguko wa pili.

Jambo ambalo limewafanya wajumbe waanze kumshangilia, huku wakisikika wakisema wagombea waanze na Yanga. ” Hawa wanaoomba ridhaa ya uongozi ndani ya Simba, muwaulize wagombea wamejiandaaje kuifunga Yanga na kuchukua ubingwa.

“Pia wagombea wote sijaona aliyetoa sela ya kuwatetea wachezaji, mfano Moses Phiri aliumizwa wangekuwa Yanga ungewasikia wanavyolalamika, lakini sisi tunanyamaza kimya.”

Ukiachana na hilo, amewaambia wagombea kwamba watakapopata ridhaa ya kuongoza wakabadilishe katiba akitolea mfano wa ibara ya 12 kifungu B kwamba mwanachama akifukuzwa haruhusiwi kuongea na asiyefukuzwa.

“Yapo mambo ya hovyo ambayo yanapaswa kubadilishwa kwenye katiba iliopo haisemi mwenyekiti anafanya kazi gani, pia mwenyekiti lazima awe na makamu wake ili akijiuzuru mwenyekiti anashika nafasi makamu wake kwa muda.

“Pia lazima mwenyekiti anayechaguliwa awe na nguvu na achaguliwe na wanachama kwa maslahi ya Simba. Na haya mambo ya wagombea kupigiwa kura na viongozi wa matawi yaondolewe kila mwanachama wa Simba apige kura,”

USIYOYAJUA KUHUSU DILI LA MUSONDA NA YANGA…TP MAZEMBE WALITAKA KUTOA MIL 279… KUHUSU HABARI ZA UBINGWA MSIMU HUU…AZAM FC KUANZA KUTUMIA MBINU ZA KIJASUSI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply