Simba SC vs Yanga SC
Habari za michezo

KISA MKUTANO WA DINI….MCHEZO WA SIMBA vs YANGA WAPANGIWA RATIBA MPYA…

admin January 23, 2023 2:18 pm

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya mabadiliko ya tarehe za michezo yote ya mzunguko wa 26 wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2022/2023 pamoja na michezo mingine miwili ya mzunguko wa 22 (Geita Gold FC dhidi ya Coastal Union FC) na (Simba SC dhidi ya Young Africans SC).

Mchezo wa Simba SC dhidi ya Yanga SC uliopangwa kuchezwa Aprili 9 utapigwa Aprili 16, 2023 katika dimba la Benjamin Mkapa.

Mchezo wa Yanga SC dhidi ya Kagera Sugar uliopangwa kuchezwa Aprili 16, 2023 utachezwa Aprili 7, 2023 katika dimba la Benjamin Mkapa.

Mchezo wa Ihefu FC dhidi ya Simba SC uliokuwa uchezwe Aprili 15 sasa utachezwa Aprili 8 katika dimba la Highland Estate.

Mchezo wa Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar uliokuwa uchezwe Aprili 15, sasa utachezwa Aprili 8, 2023 dimbani Azam Complex.

Sababu za mabadiliko hayo ni uwepo wa tukio la mkutano wa dini Aprili 9, 2023 siku ambayo ilipangwa kwa ajili ya mchezo wa Simba SC dhidi ya Yanga SC.

Mabadiliko ya tarehe ya mchezo huo yameathiri ratiba ya michezo mingine yote ya mzunguko wa 26.

ANZA WIKI KWA MICHONGO YA UHAKIKA KUTOKA MERIDIANBET…HII SIO LAZIMA MKEKA AISEE… BAADA YA ISHU YA CHAMA KUPOA…MBRAZILI SIMBA AMUANZISHIA MTITI OKRAH…AMCHANA ‘LIVE’…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply