Mkutano Mkuu simba leo
Habari za michezo

MKUTANO MKUU SIMBA:..JINA LA MANARA LATAJWA MEZA KUU…WANACHAMA WASHANGILIA…

admin January 29, 2023 5:32 pm

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala ambaye ni mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa Uchaguzi wa Simba unaofanyika leo Januari 29, amemtupia kijembe aliyekuwa Ofisa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara.

Akizungumza na Wanachama waliojitokeza katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam, Makala amesema Simba kumpa nafasi Ahmed Ally imempata mtu sahihi zaidi kuliko aliyeondoka.

“Wanasimba mnapaswa kujivunia sana kwa kupata mtu sahihi kama, Ahmed Ally kwani ameonyesha ana uwezo mkubwa wa utambuzi wa mambo,” amesema Makala akishangiliwa kwa nguvu na maelfu ya Wanachama waliojitokeza kwenye Ukumbi huo.

Manara aliyejizoelea umaarufu kabla ya kujiunga na Yanga alikuwa msemaji wa Simba.

MKUTANO MKUU SIMBA: TRY AGAIN AFUNGUKA UTAMU UNAOKUJA MSIMBAZI… KUTOKA YANGA…METACHA ‘AMVIMBISHA KICHWA’ NABI….ISHU NZIMA IKO NAMNA HII…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply