Habari za Simba SC
Habari za michezo

MKUTANO MKUU SIMBA: TRY AGAIN AFUNGUKA UTAMU UNAOKUJA MSIMBAZI…

admin January 29, 2023 5:28 pm

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salum Abdallah ‘Try Again’ amesema bado klabu hiyo ina malengo ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara licha ya kushika nafasi ya pili.

Simba ipo nafasi ya pili na pointi 50 katika michezo 21 ikiwa imeshinda michezo 15, kutoka sare michezo 5 na kupoteza mchezo dhidi ya Azam FC.

Akizungumza na Wanachama wa klabu hiyo katika Uchaguzi Mkuu unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Try Again amesema bado wana nafasi ya kuchukua ubingwa.

“Iwe au isiwe bado malengo yetu kama klabu ni kuchukua ubingwa na hilo linawezekana kwa sababu nia na uwezo wa kufanya hivyo tunao,” amesema.

Aidha Try Again alimpongeza rais wa heshima, Mohamed Dewji ‘MO’ kwa uwekezaji mkubwa alioufanya alioufanya ndani ya timu hiyo.

“Ukitaja timu 10 bora Afrika huwezi kuiacha Simba, haya ni mafanikio makubwa sana na kwa heshima nawaomba Wanachama tumpigie makofi angalau matatu Mo Dewji.

UCHAGUZI MKUU SIMBA: MANGUNGU ABADILI UPEPO …KALUWA APIGIWA YOWE UKUMBI MZIMA… MKUTANO MKUU SIMBA:..JINA LA MANARA LATAJWA MEZA KUU…WANACHAMA WASHANGILIA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply