Home Habari za michezo BAJETI YA SIMBA MSIMU UJAO HII HAPA…MO DEWJI KUCHANGIA BIL 3.9, MCHANGANUO...

BAJETI YA SIMBA MSIMU UJAO HII HAPA…MO DEWJI KUCHANGIA BIL 3.9, MCHANGANUO UKO HIVI…

Bajeti ya Simba Msimu Huu

Klabu ya Simba imetenga bajeti ya zaidi ya Sh 13.7 Bilioni mwaka 2023/2024.

Katika bajeti hiyo, Simba inatarajia kukusanya fedha kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya mapato ikiwamo udhamini.

Akisoma taarifa ya mapato na matumizi, Mkuu wa kitengo cha fedha wa klabu hiyo, Suleiman Kahumbu amesema kwenye udhamini wataingiza zaidi ya Sh 3.9 Bilioni.

“Pia Vunja Bei atatoa Sh 725 Milioni, haki za matangazo Azam Tv Sh 2.5 Bilioni na matangazo ya Ligi Sh 410 Milioni na kwenye vyanzo vinginevyo” anasema

Anasema katika bajeti hiyo,kuna upungufu wa Bilioni 3.9 ambazo rais wa heshima wa klabu hiyo, Mohammed ‘Mo’ Dewji ameitoa.

Akitoa mchanganuo wa matumizi ya bajeti hiyo anasema kwenye usajili watatumia zaidi ya Sh 2.4 Bilioni wakati mishahara ya wachezaji na wafanyakazi wengine wa klabu ni zaidi ya Sh 4.8 Bilioni.

“Bonusi kwa wachezaji ni Sh 840 milioni, leseni na vibali kwa wageni na benchi la ufundi ni Sh 189 Milioni,” anasema.

Simba pia imetenga Sh 578 Milioni za kodi ya pango, usafiri wa ndani na nje ya nchi Sh 874 milion, posho za wachezaji Sh 102milioni .

Huku ikitenga pia zaidi ya Sh 26 Milioni za matengenezo ya magari yao, Sh 500 milioni za chakula timu zao zikiwa kambini.

Suleiman aligusia bajeti ya msimu uliopita ya Sh 11.9 ambayo ilipitishwa na mkutano mkuu uliopita na kukusanya Sh 12.7 Bilioni huku Mo Dewji akiongeza Sh 2 Bilioni katika bajeti hiyo.

Msimu uliopita, klabu hiyo ilitumia zaidi ya Sh 4.38 bilioni kwenye mishahara, kambi ya wakubwa Sh 2.2 Bilioni, timu ya wanawake Sh 199 milioni.

Masuala ya utendaji zaidi ya Sh 2.6 Bilioni na malipo mengineyo Sh 385 milioni wakati usajili ulitumia Sh 1 Bilioni

SOMA NA HII  KISA MECHI ZA TIMU KUBWA....HIVI NDIVYO WAAMUZI WA BONGO WANAVYOROGWA NA KUROGANA KICHAWI....