Mshambuliaji wa Dalian Pro FC, Cesar Manzoki amekazia hoja ya kiungo mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Yanga sc kuhusu masilahi binafsi kulingana na kiwango chake uwanjani.
Manzoki wakati akiwa kwenye mkutano mkuu wa Simba SC unaliofanyika JNICC ametamka wazi kuwa kinachomfanya acheze China na sio Simba kwa wakati huu ni pamoja na kutafuta Masilahi makubwa kwasababu mpira ni karia ambayo inadumu kwa muda mfupi hivyo ni lazima atumie muda huo kukusanya fedha za kutosha ili aweze kuendesha maisha yake vizuri baada ya muda wake katika soka kumalizika.
“Viongozi walifanya kila linalowezekana nije Simba SC lakini watu wenye roho mbaya hawakutaka lakini kama nilivyosema mimi ni Mwanasimba na kama kuna klabu naweza kucheza Afrika ni Simba SC tu hakuna timu nyingine
Nipo na furaha sana na nimekuja kwenu kuwaomba baraka, kwaajili popote ambapo nitakuwepo kama sina baraka zenu ni kama mtoto ambae anaenda na hana baraka za baba, huko ambako nipo najua mnaangalia kama wazazi mnajua kuwa mpira ni karia na karia ina muda mdogo.
Kwa hiyo huo muda mdogo inabidi nifanye kitu chochote kwaajili ya kuweza kutunza familia na kufanya nyinyi wanasimba muwe na furaha ya mtoto wenu ambae nipo nje,” amesema Manzoki.
Kauli hii ya Manzoki inaenda sambamba na kauli ambayo amewahi kuitoa kiungo mshambuliaji wa Yanga SC na Taifa Stars, Fei Toto kuwa “Mpira ni maslahi na hatuchezi kwa kumfurahisha mtu, ikitokea sehemu yenye maslahi yupo tayari kwenda”.
Hivyo kinachomfanya Manzoki awepo nje ya Simba kwa wakati huu ni pamoja na kutafuta masilahi makubwa zaidi kwa maisha yake ya baadae ambayo ni sawa na hoja ya Fei Toto inayomfanya kutokuwepo kwenye kikosi cha Yanga kwa wakati huu.