Home news BAADA YA KUMALIZANA NA YANGA SC…NCHIMBI KAIBUKIA HUKU AISEE…’NI DUMA KWELI KWELI’…

BAADA YA KUMALIZANA NA YANGA SC…NCHIMBI KAIBUKIA HUKU AISEE…’NI DUMA KWELI KWELI’…

Habari za Yanga SC

Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga SC, Ditram Nchimbi amejiunga na klabu ya Fountain Gate inayoshiriki Ligi ya Championship.

Nchimbi amejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miezi sita akiwa mchezaji huru baada ya kumalizana na Yanga SC.  mshambuliaji huyo na alikiri kumalizanana Fountain huku akiweka ahadi ya kuipambania timu hiyo.

“Kweli nimesaini mkataba wa miezi sita na Fountain, walinishawishi na kuona malengo yao nini, sio tu suala la pesa bali mipango yao pia, alisema Nchimbi na kuongeza;

“Kulikuwa na timu za Ligi ambazo zimeonyesha nia ya kunihitaji lakini unaangalia wapi walipo na nikaona bora nije huku kwani tunaweza kupanda daraja.”

Usajili wa Nchimbi unamfanya aende kuungana na staa mwingine wa zamani katika Ligi Kuu, Abdulhalim Humoud ‘Gaucho’.

Nchimbi upande wa Ligi Kuu amecheza katika timu za Majimaji, Mbeya City, Azam, Polisi Tanzania na Yanga.

SOMA NA HII  NJOMBE WAPIGA HESABU ZA KURUDI LIGI KUU BARA