Home Habari za michezo BAADA YA KUWA ‘CHIMBO’ KWA MUDA MREFU…MORRISON NA AZIZI KI WAJITOKEZA YANGA…

BAADA YA KUWA ‘CHIMBO’ KWA MUDA MREFU…MORRISON NA AZIZI KI WAJITOKEZA YANGA…

Habari za Yanga

Kikosi cha Yanga  kimeendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Avic, Kigamboni Dar es Salaam kwa kucheza mechi ya mazoezi na timu ya Dar City.

Kwenye mchezo huo uliomalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0, ulitumiwa kwa benchi letu la ufundi kutoa nafasi kwa wachezaji wote waliorejea kambini.

Bao pekee la Yanga limefungwa na mshambuliaji mpya kutoka Zambia Kennedy Musonda.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imeeleza kuwa, nyota wa Yanga waliorejea kwenye mazoezi leo ni kiungo Stephane Aziz Ki raia wa Burkina Faso, winga Benard Morrison raia wa Ghana na kiungo Yanick Bangala wa Congo DR waliokuwa mapumzikoni.

Wachezaji ambao hawajaripoti kambini mpaka sasa ni Feisal Salum na beki Mamadou Doumbia.

Aidha, kikosi hicho kinaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu, dhidi ya Ruvu Shooting, utakaochezwa Jumatatu, saa 1:00 usiku katika dimba la Benjamin Mkapa.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO ...MASTAA HAWA WANNE WA SIMBA KUIKOSA AZAM FC...