Home Habari za michezo FEI TOTO TENA….AIBUKA NA DONGO JIPYA KWA YANGA….ATINGA JEZI NYUKUNDU HADHARANI…

FEI TOTO TENA….AIBUKA NA DONGO JIPYA KWA YANGA….ATINGA JEZI NYUKUNDU HADHARANI…

Kiungo wa Yanga SC Fei toto akiwa anaichezea JKU jana

Wakati Yanga, ikiingia kambini kujiandaa na mchezo wa mzunguko wa pili dhidi ya Ihefu FC, kiungo fundi wa timu hiyo, Feisal Salum ‘Fei Toto’ anaendelea kujifua Visiwani Zanzibar, huku akitokea vichochoroni na kufunga mabao sita.

Fei Toto yupo nje ya Yanga baada ya kuchukua uamuzi wa kuvunja mkataba na klabu hiyo sakata ambalo lilifanya uongozi wa timu kufungua kesi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ambao wameamuru staa huyo kurudi kwenye timu yake lakini bado anaendelea na msimamo wake.

Fei  amemshuhudiwa akifanya mazoezi na kikosi cha timu yake ya zamani JKU, ambacho kinajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Zanzibar , lakini gumzo lilikuwa idadi ya mabao aliyofunga.

Staa huyo ambaye alivalia jezi nyekundu ya timu hiyo alifika dakika tatu baada ya wenzake kuanza kupasha mwili kwa kukimbia kuzunguka uwanja.

Alivaa viatu vyake na kuomba dua kabla ya mazoezi na baadaye kuingia uwanjani kuungana na wenzake huku zogo la mashabiki wachache walioshuhudia mazoezi hayo likimyooshea kidole na kujiuliza kuwa huyu bado yupo.

Fei Toto ambaye haikujulikana amefika na usafiri gani kutokana na kutokea uchochoroni akiingia mazoezini alipasha sambamba na wenzake wakianza mazoezi saa 2:00 asubuhi hadi 3:00, alifanya programu zote zilizofanywa na timu hiyo ambayo leo imefanya mazoezi muda mchache.

Ulipofika muda wa kufunga mabao kwa mashuti ya mbali Fei Toto alikuwa gumzo baada ya kufunga mabao sita yakiwa ni zaidi ya wenzake wote waliofanya mazoezi hayo.

SOMA NA HII  KUMBE SIMBA WALITAKA WENYEWE KUTOLEWA NA AL AHLY