Home Habari za michezo KISA USAJILI WA VIFAA VIPYA …..MAYELE AANZA GUMZO YANGA…AIBUKA NA HOJA HIZI...

KISA USAJILI WA VIFAA VIPYA …..MAYELE AANZA GUMZO YANGA…AIBUKA NA HOJA HIZI MPYA…

Habari za Yanga

Wakati mabosi wa Yanga wakiendelea kuhakikisha wanamalizana na kuwatambulisha Jangwani wachezaji wawili wa kigeni mshambuliaji Mzambia, Kennedy Musonda na beki Mmali Mamadou Doumbia kabla ya dirisha kufungwa usiku wa Januari 15, mastaa wa kikosi hicho wameapa kurudi na kasi ya ajabu na kuhakikisha wanakomba kila kitu kwenye mashindano ya ndani na kufika walau nusu fainali katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Kinara wa mabao ndani ya Yanga na kwenye ligi kwa ujumla msimu huu, Fiston Mayele (mabao 14) ametaja mambo mawili ambayo anatamani kuona yanatokea msimu huu.

Amesema anaiona Yanga ikitetea tena ubingwa wa ligi msimu huu baada ya kuubeba msimu uliopita ikiwa mara ya 28 kufanya hivyo lakini pia ameweka wazi ndoto zake za kutaka kiatu cha ufungaji bora.

“Tunaongoza ligi na tupo kwenye nafasi kubwa ya kutetea ubingwa, tunajipanga zaidi kufanya vizuri kwenye kila mashindano tunayoshiriki ikiwemo ya ndani na yale ya CAF,” alisema Mayele na kuongoza;

“Pamoja na hilo, pia natamani kumaliza ligi nikiwa mfungaji bora baada ya kukikosa msimu uliopita. Naamini kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu naweza kufanikisha hilo na nitafurahi sana.”

Kiungo mpya wa kikosi hicho aliyesajiliwa kwa usajili huru, Mudathir Yahya, amesema malengo yake ni kutwaa mataji akiwa na Yanga na kampeni hiyo ataianza mara tu atakapopewa nafasi.

“Yanga ni timu kubwa, nimejiunga nayo ili kuendeleza kipaji changu na kufikia malengo ambayo miongoni mwake ni kutwaa mataji.

Nadhani kwa sasa tunapambania makombe zaidi ya mawili na kwa upande wangu kila nikipata nafasi nitajituma,” alisema Mudathir aliyewahi kuwika na Singida United na Azam FC.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA KMC