Klabu ya Yanga imetambulisha jezi mpya watakazotumia katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika 2023.
Jezi hizo tatu zimebuniwa na Sheria Ngowi na zitapatikana Jangwani Makao Makuu kwa Tsh 50,000, Ngowi amesema bluu ya nyumbani, kijani ugenini na njano third kit.
Jezi zilizozinduliwa leo ni za aina tatu, Kijani, njano na ‘Navy Blue’, ikiwa ni toleo maalum kwa ajili ya michuano ya CAF.
Aidha, Yanga SC imeingia mkataba na kampuni ya vifaa vya umeme ya #Haier kutoka China kuwa Mdhamini Mkuu wa Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika 2023.
Mkataba huo utaipa Yanga Tsh Bilioni 1.5 na Haier watakaa katika jezi za Yanga kifuani badala ya SportPesa.
Wananchi wamelazimika kumuondoa SportPesa kwa sababu Shirikisho la Soka Afrika CAF haliruhusu timu kuwa na Mdhamini ambaye ni Mshindani wa Mdhamini wa Mashindano ya CAF (1xbet).
Kwa ubunifu huu, unampa asilimia ngapi Sheria Ngowi? Ni uzi gani umeupenda zaidi?