Home Habari za michezo MTIBWA SUGAR WAIWAHI SIMBA SC….WATOA MKWARA WA KUFA MTU….

MTIBWA SUGAR WAIWAHI SIMBA SC….WATOA MKWARA WA KUFA MTU….

Msemaji wa Mtibwa Sugara, Thobias Kiafaru aitisha Simba SC

Machi 11 mwaka huu, Simba SC itaifuata Mtibwa Sugar kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa Uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro na mabosi wa klabu hiyo wamewatisha Wekundu hao wakiwaambia wafanye maombi sana ili mvua isinyeshe la sivyo wataipata freshi.

Msimu uliopita Simba SC ilivaana na Mtibwa Sugar kwenye uwanja huo katika mechi iliyopigwa Januari 22 na kumalizika kwa sare huku, Wekundu wakilalamikia hali ya uwanja iliyotokana na mvua zilizosababisha matope na safari hii wamesema hata iwenye hakutakuwa na mabadiliko ya uwanja.

Akizungumza Msemaji wa Mtibwa, Thobias Kifaru alisema si kwamba wao ndio hupanga mvua inyeshe kila inapokutana na Simba SC bali ni mipango ya Mungu, tofauti na wenzao Yanga walio na bahati kubwa ya kuutumia uwanja huo wakati kukiwa hakuna mvua kama ilivyokuwa jana.

Kifaru alisema Simba inapaswa kuomba sana ili kusinyeshe mvua, kwani kwa hali yoyote hawatawabadilishia uwanja na kilichowakuta msimu uliopita itakuwa maradufu kwani safario hii hawataki sare nyumbani.

β€œNi imani tu kuwa Yanga ikicheza huku basi mvua huwa inafungwa na wazee, hiyo ni kutia ladha tu ya mechi kila kitu ni mipango ya Mungu, Simba SC walikuja kipindi ambacho mvua inanyesha hivyo wamuombe Mungu watakapokuja wakutane na hali ya hewa nzuri.

β€œHatuna mpango wa kubadilisha uwanja, mechi zetu zitapigwa hapa hapa na tunaendelea kuuboresha uwanja wetu uwe wa kisasa zaidi, waombe tu neema ya Mungu wasikutane na mvua vinginevyo itawasumbua tu,” alisema Kifaru

SOMA NA HII  EDO:- VIONGOZI SIMBA WANARUDIA SANA MAKOSA ....HAWAJUI TATIZO LILIPO..