Home Habari za michezo RAGE : WANASHERIA WA FEI TOTO HAWTAUMII SHERIA ZA FIFA….WANAHANGAIKA…

RAGE : WANASHERIA WA FEI TOTO HAWTAUMII SHERIA ZA FIFA….WANAHANGAIKA…

Habari za Yanga

Wakati Sakata la Kiungo wa Yanga Feisal Salum “Fei Toto” likizidi kuchukua sura mpya kila leo huku wengi wakiwa hawajui mwisho wake.

Bado ufafanuzi umeendelea kutolewa na wenye ufahamu na masuala hayo ya kisheria kwa pande zote mbili za FIFA na Sheria za nchi.

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba SC, Ismail Aden Rage amesema wanasheria wa mchezaji, Feisal Salum wanatumia sheria za kawaida za kazi na siyo sheria za mpira zilizowekwa na FIFA

“Sheria za nchi mfanyakazi anaweza akavunja mkataba wakati wowote lakini alipe mshahara wa miezi 3 hiyo ni sheria ya kazi ya Tanzania lakini timu za mpira zinabanwa na sheria za FIFA.”

Mpaka sasa bado Feisal Salum hajaripoti katika kambi ya Yanga huku Kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji ya TFF wakitoa taarifa kuwa ni mchezaji halali wa Yanga.

SOMA NA HII  BALAA ZITO NI KUSAKA USHINDI KWA NAMNA YEYOTE