Wachezaji wa Horoya wahaidiwa milioni 11 kuifunga Simba
news

WAGUINEA WAIPANIA SIMBA….KILA MCHEZAJI KUJAZWA MILIONI 11 MNYAMA AFE MAPEMA…

admin February 11, 2023 4:41 pm

Klabu ya Horoya imeahidi kiasi cha $5000 (Tsh. Milioni 11. 6) kwa Kila mchezaji endapo wataibuka na alama tatu dhidi ya Simba SC hii leo katika mechi yao ya kwanza ya hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika msimu huu.

Bodi ya Klabu hiyo pia imeahidi kiasi cha USD $10,000 (Tsh. Milioni 23.3) kwa kila mchezaji kama watapata ushindi dhidi ya Raja Casablanca .

Horoya na Simba zinakutana jioni ya leo katika mchezo wa pili wa kundi C, ambapo mchezo wa kwanza ulipigwa jana Kwa Raja Casablanca kuifunga Vipers ya Uganda magoli 5-0.

Kwa matokeo ya jana , Raja Casablanca wanaongoza msimamo wa kundi C wakiwa na alama 3 pamoja na magoli 5, huku Simba wakiwa ni wapili kwa kuzingatia viwango vya CAF.

Matokeo ya zaidi ya magoli 5 kwa Simba leo hii, yataifanya kuishusha Raja Casablanca kileleni na kuukalia usukani wakundi mpaka mechi ijayo ambayo Raja Casablanca watakuwa wageni wa Simba jijini Dar es Dar es laam.

BAADA YA KUONA VIPERS WAMEBONDWA JANA…MBRAZILI SIMBA AIBUKA NA HILI JIPYA KWA HOROYA… FIFA WAIBUKA NA HILI JIPYA SAKATA LA MABILIONI YA MSUVA KUTOKA KWA WAARABU….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply