Habari za Simba leo
Habari za michezo

BAADA YA KUTOONEKANA SANA….SIMBA WAFICHUA ALIPO MKUDE…

admin February 16, 2023 2:36 pm

Afisa Habari wa Klabu ya Simba Ahmed Ally amefafanua suala la Kiungo wa Wekundu wa Msimbazi Jonas Mkude kukosekana kwa muda mrefu kwenye kikosi cha Simba huku akisema katika mchezo wa Raja Casablanca atakuwa sehemu ya mipango ya Kocha Robertinho.

Akizungumza kwenye kipindi cha Sports Arena cha Wasafi FM jana Februari 15 katika kampeni ya kuhamasisha mashabiki kuipa nguvu timu yao kwenye mchezo huo wa Kimataifa, utakaopigwa siku ya Jumamosi Februari 18, 2023.

“Kwenye mchezo wa Horoya Mkude hakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kwakuwa Kocha Robertinho alikuwa na machaguo ya viungo wengi, kama Mzamiru na Sadio Kanoute hivyo kukosekana kwa Kanoute ni moja kwa moja atakuwa kwenye mipango wa Mwalimu dhidi ya Raja Casablanca” Ahmed Ally.

Aidha aliongeza kuwa katika mchezo huo klabu ya Simba itaingia na matokeo ya ushindi tu licha ya mpira kuwa na matokeo matatu.

“Mpira una matokeo matatu, kufunga, kufungwa na kutoa sare, lakini kwenye mchezo wa Jumamosi dhidi ya Raja Casablanca hatutaingia na matokeo matatu, Simba itaingia na matokeo ya aina moja tu ya kushinda mechi hiyo” Ahmed Ally

YANGA WAPINDUA MEZA KIBABE KWA FEI TOTO…WAMALIZANA NAYE MAZIMA..SASA KUPEWA MSHAHARA ML 15.. NABI:- YANGA HATUTARUDIA MAKOSA KWA MAZEMBE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply