Habari za michezo

HUU HAPA UNDANI WA AJALI YA FEI TOTO JANA AKIWA ZNZ….POLISI WAANIKA KILA KITU A-Z…

admin February 16, 2023 10:31 am

Mchezaji wa Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania Feisal Salum Abdallah (Fei toto) amepata ajali mchana wa jana Fuoni, Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar.

Ajali hiyo imehusisha Gari yake aina ya Harrier nyeupe yenye namba za usajili Z 160 MW huku dereva akiwa ni mwenyewe Feitoto akitokea Fuoni kituo cha zamani akielekea Mjini ndipo ilipogongana na Bodaboda yenye namba za usajili Z 423 KL.

Katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha wala kuumia zaidi ya Gari kuharibika mbele na Bodaboda imeharibika ambapo mpaka sasa Vyombo hivyo vipo kituo cha Polisi Fuoni .

“Ni kweli imetoka ajali hapa Fuoni Gari aina ya Harrier imegongana na Bodaboda, Gari ni ya yule bwana mdogo mchezaji wa Yanga Fei, lakini ni ajali ndogo tu hakuna aliyeumia”-Mkuu wa Kituo Cha Polisi Fuoni.

BAADA YA KUMALIZANA NA WATUNISIA… MKAKATI WA YANGA ‘KUIPELEKEA MOTO’ MAZEMBE UKO HIVI… WAKATI MAN U NA BARC ZIKIUMANA ..TUMIA FURSA YA ODDS BOMBA ZA MERIDIANBET KUTUSUA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply