Habari za Yanga
Habari za michezo

KISA YANGA KUICHAPA MAZEMBE JANA…NABI AWAPIGA KIJEMBE SIMBA…

admin February 20, 2023 9:21 pm

Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia Nasreddine Nabi amesema ushindi walioupata dhidi ya TP Mazembe hauhusiani na kipingo walichokipata watani wao wa jadi Simba Sc katika mechi yao ya CAFCL dhidi ya Raja Casablanca ambapo Wekundu hao walifungwa bao 3-0 wakiwa nyumbani.

Nabi amesema hayo jana Jumapili, Februari 19, 2023 wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya mchezo wa yanga dhidi ya TP Mazembe ya Congo DR ambapo Yanga aliibuka na ushindi wa bao 3-1.

“Matokeo ya Simba jana (juzi) dhidi ya Raja Casablanca sio chachu ya kwetu sisi kucheza vizuri katika mchezo wa leo (jana). Simba inawakilisha Tanzania, Yanga pia inawakilisha Tanzania. Sisi kama benchi la ufundi tuliangalia makossa tuliyofanya, hata wanahabari walitusema sana.

“Tangu nianze kufundisha, ile mechi ndiyo mechi yangu ya kwanza kucheza katika kiwango ambacho sikutarajia. Hii ilitufanya sisi kama benchi la ufundi kurudi na kuangalia wapi yalipokuwa mapungufu yetu na jinsi ya kuyafanyia kazi ili tuendelee kufanya vizuri,” amesema Kocha Nabi.

BAADA YA SAWADOGO KUYUMBA MECHI NA WAMOROCCO…MBRAZILI SIMBA ASHUSHA PUMZI NA UJIO WA KANOUTE… KISA KUFUNGWA NA RAJA…SIMBA WAMVUTIA WAYA KOCHA MSOMI…MAZEMBE WASEPA NA BANGALA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply