Habari za michezo

UMESIKIA HIYOO…TIMU ITAKAYOMTAKA ‘JINI’ HAALAND IWE NA TSH TRILIONI 2 ….

admin February 23, 2023 7:05 am

Umeseikia hiyo, thamani ya staa wa Manchester City, Erling Haaland kwa sasa ni euro bilioni 1 sawa na zaidi ya Tsh Trilioni 2 za kitanzania.

Haya yameelezwa na wakala wa staa huyo, Rafaela Primenta ambaye anamsimamia Haaland na mastaa wengine akiwemo Paul Pogba, Marco Verratti, Gianluigi Donnarumma, Matthijs de Ligt.

Staa huyo ndani ya Manchester City kwenye Premier msimu huu amefanikiwa kufunga mabao 26, huku Ligi ya Mabingwa Ulaya akifunga mabao matano katika mechi nne.

Pimenta alisema: “Erling Haaland kwa sasa thamani yake ni euro bilioni 1 na kwenye hili nipo siriazi, hii ndiyo thamani yake.

“Kuhusu hatma ya Marco Verratti, kwa kweli ni ngumu kuona anakwenda katika klabu nyingine, anaipenda Paris Saint-Germain na anataka kuwa pale.”

Ikumbukwe kuwa, licha ya Haaland kutua ndani ya Manchester City msimu huu, lakini bado staa huyo anawindwa na klabu kubwa kama Real Madrid.

BAADA YA KUSIKIA YANGA WALICHOIFANYWA MAZEMBE DAR…REAL BAMAKO WAGUNA KISHA WAKASEMA HILI… YANGA WAIFUNGA REAL BAMAKO WAKIWA DAR…HIVI NDIVYO NABI ALIVYOCHEZA KETE ZAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply