Neo Maema Kutua Leo Kukamilisha Usajili Simba SC, Mchezaji Mmoja Akatwa Cheti!
DAR ES SALAAM: Kiungo mshambuliaji wa kimataifa kutoka Afrika Kusini, Neo Maema, anatarajiwa kuwasili nchini leo kukamilisha kurejea kwake katika klabu ya Simba SC kwa mkataba wa mkopo wa msimu mmoja kutoka Mamelodi Sundowns. Uamuzi huo ni sehemu ya mikakati ya Wekundu wa Msimbazi kujiandaa kikamilifu kuelekea msimu mpya wa 2026/27.
Urejeo wa Maema unakuja baada ya uongozi wa Simba kufikia makubaliano ya mwisho na Mamelodi Sundowns. Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker, ameweka wazi kuwa alihitaji kwa kiasi kikubwa huduma ya nyota huyo ili kuongeza ubora, kasi, na ushindani wa namba katika safu yake ya kiungo.
Barker anaamini uzoefu, uwezo wa kutengeneza nafasi, na ubunifu wa Maema utakuwa chachu kubwa kwa Simba katika harakati za kutwaa mataji ya ndani pamoja na kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa.
Maema anarejea Msimbazi akiwa na kumbukumbu nzuri za kiwango cha juu alichokionyesha kwenye kipindi chake cha awali, ambapo alikuwa nguzo muhimu kwenye safu ya ushambuliaji na kutengeneza mabao.
Alassane Kante Kuondoka? Hata hivyo, ujio wa kiungo huyo unatarajiwa kuleta mabadiliko kwenye kikosi cha wachezaji wa kigeni. Taarifa kutoka ndani ya klabu zinaeleza kuwa kurejea kwa Maema kutafungua mlango wa kuondoka kwa mshambuliaji Alassane Kante, ili kupisha na kutimiza kanuni za usajili wa idadi ya wachezaji wa kigeni inayotakiwa.