Habari za Simba
Habari za michezo

FUKO LA PESA LA RAIS SAMIA LAFANYA KWELI…SIMBA WAPOKEA MAMILIONI YA PESA…

admin February 26, 2023 6:05 pm

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa leo Februari 26 2023 amewakabidhi Simba SC kitita cha shilingi milioni 5 ikiwa ni ahadi ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kutoa milioni 5 kwa kila goli litakalofungwa na wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa ambao ni Simba na Yanga SC.

Simba jana Februari 25,2023, walifanikiwa kuwafunga goli 1-0 Vipers FC ya Uganda na kuweka kibindoni alama tatu baada ya kucheza michezo miwili ya awali kuambulia kichapo ikiwa ni hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika.

Kwenye Kundi lao, Simba wanakamata nafasi ya tatu, juu yao wakiwa Horoya wenye pointi nne huku Raja Casablanca wakiwa vinara wa Kundi lao wakiwa na pointi 9. Vipers sasa wanakamata mkiwa wakiwa na alama moja pekee.

KUELEKEA MECHI YA SHIRIKISHO LEO…REKODI YA YANGA CAF YASHTUA AFRIKA…KAZI IKO HAPA… KISA UDHAIFU WA  REAL BAMAKO…MAYELE AIONA ROBO FAINAL CAF…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply