Jezi Mpya za Simba Kimataifa
Habari za michezo

JEZI MPYA ZA SIMBA ZATUA RASMI BONGO….

admin March 3, 2023 1:42 pm

Baada ya kusuasua kwa muda mrefu, hatimaye jezi mpya za Simba SC, zimewasili nchini tayari kwa ajili ya kuanza kuuzwa kwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo.

Akizungumza na wanahabari leo Marchi 3, 2023, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally, amesema jezi hizo maalum kwa mashindano ya Kimataifa zilizoandikwa Visit Tanzania zimewasili na zinapatikana kwenye maduka yote ya Vunja Bei.

“Kama tilivyokuwa tunaulizana zitafika lini, tayari zimefika na sasa twendeni tukazinunue zinapatikana kwenye maduka yote ya Vunja Bei kwa shilingi elfu thelathini na tano tu.

“Ukinunua moja unapata na tiketi ya bure ya mzunguko na utaweza kwenda kushuhudia mchezo wetu ujao dhidi ya Vipers utakaopigwa katika dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar, Marchi 7,” alisema Ahmed.

Jezi hizo zilikuwa ziwasili nchini kabla Simba haijaanza kucheza mechi za hatua ya makundi lakini ilielezwa kuwa zilishindikana kufika kutokana na kukwama nchini Ethiopia kutokana na changamoto ya kiusafiri.

JULIO:- AZAM FC WANIPE TIMU TUSHINDE LIGI KUU MIAKA KUMI MFULULIZO… KISA MGUNDA…JULIO AWASHUKIA MABOSI WA SIMBA….AFUNGUKA KUHUSU NAFASI YA MBRAZILI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply