Simba vs Raja
Habari za michezo

AHMED ALLY: BAADA YA KUPIGWA NA RAJA…SIMBA NZIMA TULIKATA MOTO…HATUWAWEZZI WALE..

admin March 4, 2023 9:35 pm

Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally amesema, kwenye mechi yao ya pili ya Hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa walikata moto baada ya kufungwa goli la tatu na Raja Casablanca.

Ahmed alisema, siku hiyo alikuwa hafatilii mechi bali zaidi alikuwa akiangalia jinsi ambavyo mashabiki wanashangilia kabla na hata baada ya kufungwa.

“Ukweli ni kwamba Raja hatuwawezi kwa kushangilia lakini siku ile walibebwa zaidi na ushindi wao, laiti tungewafunga sisi, wale wangeloa lakini bahati mbaya walipotufunga wao ndipo na sisi tukakata moto hasa baada ya kufungwa goli la tatu,” alisema Ahmed.

Simba wanatarajia kuwakaribisha Vipers SC Marchi 7, 2023 kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar ikiwa ni mchezo wa marudiano baada ya wa awali kushinda 1-0 ugenini.

KUHUSU SAKATA LA FEI TOTO…FATUMA KARUME AIBUKA NA HILI…ATAJA UTUMWA… WAARABU WAPANIA KUMNG’OA NABI YANGA….TP MAZEMBE NAO WAMTAKA…MAYELE ‘ATEMBEA’ NA  BEKI WA SIMBA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply