Habari za Simba
Habari za michezo

MASTAA SIMBA WAFUNGIWA KUIWINDA VIPERS ….VIGOGO WAPANIA KUMALIZA KAZI MAPEMA….

admin March 5, 2023 7:01 am

Wekundu wa Msimbazi Simba SC,  wameingia rasmi kambini kuwawinda Vipers wa Uganda mchezo wa marudiano wa Hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika.

Simba wanatarajia kumenyana na Vipers Jumanne ijayo Marchi 7, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema, wachezaji wameingia kambini rasmi  na wanatarajia kuanza mazoezi jioni.

“Huwa tunaanza kambi kabla ya siku tatu au nne kabla ya mchezo lakini kwa kutambua umuhimu wa mchezo huu, tumeanza kambi siku tano kabla ili kuwa tayari zaidi kutokana na ugumu wa mchezo wenyewe.

“Vipers nao watakuja wakiamini kwamba wanaweza kupata nafasi ya kuvuka japo nafasi yao ni finyu lakini wanaamini wanaweza kutoboa, tumenza kambi mapema ili kukabiliana nao,” alisema Ahmed.

ZITTO:- YANGA NA TFF WANAWAZA NINI KWANI….FEI TOTO ASILAZIMISHWE..APIGWE FAINI AENDE ATAKAPO… BAADA YA YANGA KUWAIGA KILA JAMBO….SIMBA WAJA NA HILI JIPYA KUHUSU ‘KISPIKA MTAANI’….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply