Ahmed Ally Simba SC
Habari za michezo

BAADA YA YANGA KUWAIGA KILA JAMBO….SIMBA WAJA NA HILI JIPYA KUHUSU ‘KISPIKA MTAANI’….

admin March 5, 2023 7:15 am

Simba SC imebadili staili ya kuhamasisha mashabiki wake kuelekea mchezo wao wa Kimataifa dhidi ya Vipers SC utakaochezwa Jumanne ijayo, Marchi 7, 2023 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

Ahmed Ally amesema, Jumapili hii watakuja na hamasa ya Kibichibichi ambapo, mashabiki na wanachama wa Simba, watakutana kwnye fukwe za Coco Beach jijini Dar kula bata na kuhamasishana kuhusu mchezo huo.

“Kispika kinakuja kwa staili nyingine, tutakutana Coco Beach pale tunakula bata tukiwa tumevalia jezi zetu za Simba, tunakula mihongo huku tunapart huku tukihamashishana,” alisema Ahmed.

Mbali na hilo, Simba pia wamekuja na staili mpya ya kuuza tiketi maalum za mchezo huo kwa kuwafuata mashabiki wapya kwenye makampuni mbalimbali kisha kuwahamaisha wanunue tiketi maalum zitakazowawezesha wafanyakazi wa makampuni kwenda kushuhudia mechi hiyo.

MASTAA SIMBA WAFUNGIWA KUIWINDA VIPERS ….VIGOGO WAPANIA KUMALIZA KAZI MAPEMA…. SIKU CHACHE BAADA YA KULA KIAPO MBELE YA RAIS SAMIA…SIMBA WAMUWAHI ‘MWANA FA’…WAMPA JUKUMU HILI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply