Habari za Yanga
Habari za michezo

WINGA TELEZA WA TP MAZEMBE AKUBALI KUTUA YANGA…NI YULE ALIYEMTESHA ULIMI DJUMA

admin March 9, 2023 6:54 pm

Jina la Phillipe Kinzumbi wala sio geni katika kumbukumbu za mashabiki hapa nchini, hiyo ni kutokana na ubora mkubwa aliuonyesha mchezaji huyo wa TP Mazembe walipokutana na Yanga katika Uwanja wa Mkapa.

Kinzumbi katika mchezo huo licha ya timu yake ya Mazembe kufungwa mabao 3-1, lakini aliwashawishi mashabiki wa Yanga mara baada ya kumtesa beki wao, Lomalisa Mutambala kiasi cha kupendekeza winga huyo awe katika mipango ya usajili wa dirisha kubwa.

Winga ametuambia, kuwa yupo tayari kukipiga ndani ya Yanga lakini kwa masharti ya viongozi wa Yanga waende mezani kuzungumza na uongozi wa timu yake na kama mambo yataenda sawa basi yeye hana shida na atajiunga na miamba hiyo ya Tanzania.

“Mimi siwezi kusema vitu vya usajili kwa sasa kwa kuwa mimi ni mchezji wa TP Mazembe, Yanga ni timu nzuri na ina mashabiki wengi ambao wanapenda sana mpira hivyo naamini kwa mchezaji yoyote lazima uvutiwe na timu ya namna hiyo.

“Siwezi kusema kuwa sitaki kuja kuwa mchezaji wa Yanga hapana kuna utaratibu unatakiwa utumike, viongozi wa Yanga wakafanye maazungumzo ya usajili wangu na kama kutakuwa na makubaliano basi mimi sina neno na nitakuja kucheza huko.

“Unajua kwa sasa Yanga sio sehemu ya kufikiria kutokana na kuwa kama nyumbani pale, kuna familia yetu kubwa ya mpira ipo pale, kina Moloko, Kisinda, Djuma, Bangala na Mayele wote wapo pale na hao wote ni familia yetu ya mpira hivyo ni kama nyumbani tu DR Congo,” alimaliza winga huyo.

NABI:- AZIZ KI HAKUCHEZA KWA MASLAHI YA YANGA…HAKUWA BORA KWANGU … VIGOGO TFF WAFICHUA ‘MADUDU’ YA FEI TOTO….AAMBIWA ATAJE TIMU ANAYOTAKA KWENDA JAMBO LIISHE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply