Habari za Yanga
Habari za michezo

KISA MAYELE NA MUSONDA…YANGA WATUMA UJUMBE HUU KWA CAF….MATAKWA YAO HAYA HAPA…

admin March 13, 2023 11:42 am

Kiwango bora kinachoendelea kuoneshwa na Yanga katika mashindano mbalimbali msimu huu, kimemuibua Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said ambaye ameweka wazi kuwa, wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri na kuandika historia mpya katika Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.

Yanga ambao jana Jumapili walikushuka kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar, kuvaana na Geita Gold katika mchezo wa wa Ligi Kuu Bara, ndio wawakilishi pekee wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika wakiwa Kundi D.

Yanga wamekuwa kwenye kiwango bora msimu huu ambapo baadhi ya mastaa wa kikosi hicho akiwemo Fiston Mayele na Kennedy Musonda, wakionesha uwezo mkubwa katika mashindano tofauti.

Kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi, Mayele na Musonda wamechangia mabao matatu mpaka sasa.

Akizungumza nasi, Injinia Hersi alisema: “Tunafurahia ubora wa kikosi chetu na matokeo ambayo tumeendelea kuyapata, hii inaonesha ni kwa kiasi gani kama timu tumeamua kufanya makubwa msimu huu.

“Kwenye Kombe la Shirikisho Afrika tuna nafasi nzuri ya kucheza robo fainali ikiwa tutaibuka na ushindi dhidi ya US Monastir, tunaamini kuwa kwa ubora wa kikosi tulionao tunaweza kuandika rekodi katika mashindano ya Afrika msimu huu.”

KUHUSU MZIZA NA NAMNA ANAVYOCHEZA YANGA…NABI KATIKISA KICHWA WEE..KISHA AKASEMA HAYA… BAADA YA KUWATAZAMA SIMBA WANAVYOCHEZA…PATRICK PHIRI KAGUNA KISHA AKAWASHTUA MABOSI MSIMBAZI KWA HILI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply