Home Habari za michezo ZA NDAANI KABISA…SIMBA WAANZA USAJILI MAPEMA….MBADALA WA TSHABALALA HUYU HAPA…ANAPIGA KROSS BALAA…

ZA NDAANI KABISA…SIMBA WAANZA USAJILI MAPEMA….MBADALA WA TSHABALALA HUYU HAPA…ANAPIGA KROSS BALAA…

Habari za Simba SC

Simba juzi jioni ilikuwa Uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro kumalizana na Mtibwa Sugar katika mechi ya Ligi Kuu Bara kisha kuanza kujipanga kwa mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya ya Guinea, huku mabosi wa klabu hiyo wakianza usajili wa msimu ujao kimyakimya.

Mabosi wa Simba wamekiangalia kikosi hicho kilivyo kwa sasa na kuona kuna maeneo yenye uhitaji wa kuimarishwa mapema kwa ajili ya msimu ujao na fasta wameanza na beki wa kushoto, Yahya Mbegu anayekipiga kwa sasa Ihefu SC ambaye mkataba wake ukitarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.

Habari kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa mazungumzo baina ya pande hizo mbili yapo kwenye hatua nzuri ikielezwa kwamba Mbegu aliyewahi kukipiga Polisi Tanzania ndiye chaguo sahihi la kumpa ushindani Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ anayemiliki beki ya kushoto Msimbazi kwa muda mrefu.

Inaelezwa kuwa mabosi wa Simba wameanza mazungumzo na menejimenti ya mchezaji huyo ili msimu ujao atue kuvaa uzi wa timu hiyo katika mechi za Ligi Kuu Bara, Kombe la ASFC na michuano ya CAF.

Mbegu yupo kwenye mipango ya Simba kwa muda mrefu, lakini awali dili lilikwama na lengo la kutakiwa Msimbazi ni kwenda kumsaidia Tshabalala na huenda ujio wake ukatoa nafasi kwa Gadiel Michael ambaye amekuwa akianzia benchi kufunguliwa mlango wa kuondoka klabuni.

Beki huyo mkali wa kupiga krosi alisajiliwa na Ihefu katika dirisha dogo la usajili akitokea Polisi Tanzania na amekuwa akionyesha uwezo mkubwa katika michezo anayocheza akitengeneza ukuta wa timu hiyo iliyopo Mbarali mkoani Mbeya – timu pekee iliyoifunga Yanga msimu huu katika Ligi Kuu.

Mmoja wa mabosi wa Simba aliyekataa kutajwa jina gazetini alisema wamemfuatilia kwa muda mrefu mchezaji huyo na kugundua ni mzuri na ana uwezo mkubwa wa kusaidiana na Tshabalala.

Mbegu aliyewahi kuzichezea Geita Gold na Mwadui alipoulizwa  juu ya kuwepo kwa dili la kutua Msimbazi, alikiri kuwepo kwa jambo hilo akisema lolote linaweza kutokea na suala hilo lipo katika menejimenti yake.

“Kwa sasa ni mchezaji wa Ihefu, lakini kama suala hilo lipo au la wenye wajibu wa kulielezea ni menejimenti yangu, ila kwa mchezaji yeyote mwenye malengo makubwa lolote linaweza kutokea. Lakini ni lazima ujue kwa sasa ligi inaendelea na nina mkataba na klabu yangu,” alisema beki huyo aliyeichezea timu ya vijana ya Simba na timu ya taifa ya vijana U20.

SOMA NA HII  UFINYANGE MKEKA WAKO LEO KWA KUZINGATIA ODDS ZA KWENYE TIMU HIZI...