MAAFANDE WATEMBEZA KIPIGO...WANYEMELEA LIGI KUU...KITUO KINACHOFUATA PAMBA FC
Habari za michezo

MAAFANDE WATEMBEZA KIPIGO…WANYEMELEA LIGI KUU…KITUO KINACHOFUATA PAMBA FC

Marce Ben Komba March 15, 2023 2:24 pm

Huko Championship Maafande wa JKT Tanzania wanazidi kufanya yao kuhakikisha msimu ujao wanacheza Ligi Kuu baada ya kuendeleza vichapo kwenye ligi hiyo.

JKT Tanzania sasa imefikisha alama 53 na kuweka pengo la alama 11 kati yake na Kitayosce FC inayoshika nafasi ya pili huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Maafande hao wamepoteza michezo miwili tu msimu huu, katika michezo 21 waliyocheza.

Vijana hao wanaonolewa na Malale Hamsini wamesalia na mchezo saba kumaliza ligi dhidi ya Pamba FC.

Katika michezo hiyo, JKT Tanzania inasaka alama 12 sawa na michezo minne pekee kujihakikishia kucheza Ligi Kuu msimu ujao.

YANGA IMEUPIGA MWINGI…IMEMSAJILI FUNDI MALI….WAMALIZANA NAYE HOSPITALI AZAM FC DAWA IMEPENYA HASWA…KOCHA ANASIKITISHA HAKUTARAJIA…MBIO ZA UBINGWA BYE BYE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply