Habari za Yanga
Habari za michezo

BAADA YA UKIMYA MREFU….HATMA YA NKANE YANGA YATUPWA KWA NABI…ISHU NZIMA IKO HIVI…

admin March 16, 2023 9:12 pm

Kiungo Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Yanga Denis Nkane tayari amerejea katika mazoezini ya kikosi cha klabu hiyo, baada ya kupona majeraha ya nyonga yaliyomuweka nje tangu mwishoni mwa mwezi Desemba, mwaka jana na sasa anamsikilizia kocha mkuu, Nassredine Nabi ampe nafasi kuanza kukiwasha.

Nkane alikaa nje kwa kipindi kisichopungua wiki sita akiuguza jeraha hilo la nyonga ambalo Daktari wa Yanga, Moses Etutu alithibitisha ilivunjika mfupa mdogo na kusababisha nyonga kujikunja lakini sasa yupo fiti na tayari kwa mapambano.

Akizungumza baada ya kufanya mazoezi kwa siku kadhaa za kikosi cha kwanza cha Yanga Nkane amesema “Niko poa sasa na siku yeyote mtaniona uwanjani nikicheza kwani nimepona tayari.”

Mbali na kiungo huyo, pia imethibitika kuwa Benard Morrison aliyekuwa nje tangu mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka huu akiuguza jeraha la nyonga, ameanza mazoezi mepesi, na wakati wowote ataungana na wachezaji wengine kwa mazoezi ya pamoja.

YANGA:- WAACHENI WAARABU WAJE WANATAKA DAWA…HIVI WALITUFUNGAJE? WALIBAHATISHA…MASHABIKI NJOONI NA SANDA AHMED ALLY AWACHANA CHAMA,MANULA NA KAPOMBE…PUNGUZENI MAKOSA,TUMIENI NAFASI…AMPIGIA SALUTI KIPA VIPERS

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply