Habari za Yanga SC
Habari za Usajili

YANGA IMEFUNGIWA USAJILI?…KWA KUFULI GANI!…WANATUFANYIA FIGISU FIGISU

Marce Ben Komba March 17, 2023 5:30 am

Wakati Taarifa zikiibuka mchana wa leo kuwa Klabu ya Yanga
imefungiwa kufanya usajili kwa misimu mitatu kutokana na kutomlipa aliyekuwa Kocha wake Luc Eymel stahiki zake baada ya kumvunjia Mkataba kinyume na taratibu.

Viongozi mbali mbali wa Yanga wameibuka na kuwataka
wanachama, Mashabiki na wapenzi wa Yanga kupuuza taarifa hizo na kuziita propaganda.

FIFA wana utaratibu wao rasmi wa kutoa taarifa kuhusu jambo lao. Anapotokea mtu kusema Yanga wamefungiwa kusajili madirisha matatu, aseme tumefungiwa na kufuli gani?

Taarifa hawajaitoa FIFA, Luc au Yanga ambao ndio wahusika wa jambo hilo,hiko chombo kimetoa wapi taarifa?” amezungumza Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga Patrick Simon kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika;

“Jumapili tuna mchezo muhimu sana, nawaomba Wanachama, Wapenzi na Mashabiki tusitolewe mchezoni na habari za kizushi.

Taarifa za Yanga kufungiwa ni mwendelezo ule ule wa uvivu wa kufanya utafiti na kufatilia mambo kwa undani kwa baadhi ya waandishi wa hii nchi.
Tuendelee kununua tickets zetu, Jumapili tukutane mapema kwa Mkapa

YANGA YAPEWA SIKU 45 NA FIFA…YATAKIWA KULIPA DENI…ITAFUNGIWA USAJILI MISIMU MITATU CLATOUS CHAMA…MIMI KAMA MCHEZAJI SINA MANENO MENGI…NITAONYESHA VITENDO ZAIDI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply