Habari za michezo
BAADA YA KUPIGWA MBILI KAVU JUZI NA YANGA…WAARABU WAIBUKA NA HILI JIPYA….WAITAJA CAF…
Rais wa Klabu ya US Monastir kutoka nchini Tunisia, Ahmed Belli, ameipongeza Young Africans kwa kufuzu hatua ya Robo Fainali kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Jumapili (Machi 18), Young Africans ilipata ushindi wa mabao 2- O dhidi ya US Monastir kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, na kufuzu hatua ya Robo Fainali.
Belli amesema: “Tumepoteza mchezo wetu mbele ya Young
Africans, yote haya ni matokeo ya mpira wa miguu, tunachoangalia sasa ni namna gani tutakavyojiandaa kwa ajili ya mechi za hatua ya Robo Fainali.“Nawapongeza sana Young Africans kwa kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza katika michuano hii, nawatakia kila la kheri kwenye hatua ya robo fainali na naamini watafanya vizuri zaidi ya walivyofanya katika hatua ya makundi.”
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.