Habari za Yanga
Michezo

WANAOKUSHANGILIA WATAKUJA KUKUCHEKA…KIUNGO SIMBA AMSHAURI FEISAL SALUM “FEI TOTO”

Marce Ben Komba March 21, 2023 4:36 pm

Akiwa na Takriban miezi minne pasipo kucheza mpira kutokana na mgogoro wa Kimkataba biana yake na Klabu yake ya Yanga huku taarifa za uhakika zikidai ni kudai maslahi.

Mchezaji wa Yanga, Kiungo Feisal Salum “fei toto” amepewa mbinu namna ya kupata maslahi anayoyadai kupitia kipaji chake.

Kiungo wa Simba anaeikipiga kwa Mkopo Ihefu, Mnigeria Victor Akpan, amemshauri Feisal namna ya kulipwa pesa ndefu kwa wachezaji wa kigeni.
Akizungumza Akpan amesema;

“Kuhusu Fei Toto, Mimi kama mchezaji ninayejua mchezo wa mpira ni wa muda mfupi naelewa anachopitia, wanaomshangilia leo akiwa staa watamcheka akistaafu kama hajajiwekeza kimaisha.

“Huenda kweli kakosea kuvunja mkataba, lakini Yanga wanaionaje thamani ya Fei Toto maana kwa sasa yupo kwenye kiwango cha juu asipopewa anachokitaka atapewa nyakati zipi, soka lina mambo mengi sana.”

YANGA “HATUMUOGOPI MTU…TUNAMSUBIRI YOYOTE…LIGI YA MABINGWA AFRIKA MSUVA AWAKANA YANGA…SIMBA NI KLABU KUBWA AFRIKA…INAFANYA VIZURI LIGI YA MABINGWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply