YANGA YATOA SIRI NZITO USAJILI WA MUSONDA...ULE NI USAJILI WA KIMKAKATI
Michezo

YANGA YATOA SIRI NZITO USAJILI WA MUSONDA…ULE NI USAJILI WA KIMKAKATI

Marce Ben Komba March 24, 2023 9:26 am

Uongozi wa Yanga umeweka wazi kuwa usajili wa nyota wa Zambia, Kennedy Musonda ni wa kimkakati kutokana na jicho lake kwenye kufunga.

Musonda ameibuka ndani ya Yanga akitokea kikosi cha Power Dynamo ya Zambia ikiwa ni moja ya usajili wa dirisha dogo uliojibu kwenye anga la kimataifa.

Ni mabao mawili kafunga mwamba huyo, alianza kutupia dhidi ya TP Mazembe kisha US Monastir kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ambayo yamesaidia Yanga kutinga robo fainali ya michuano hiyo.

Akizungumza nasi, Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga alisema kuwa, kazi ni kubwa inayofanywa na Musonda akishirikiana na wachezaji wengine.

“Kila mchezaji anatimiza majukumu yake lakini Musonda huyu aliletwa maalumu kwa ajili ya mechi za kimataifa hilo ni jambo ambalo linaonekana kwa sasa.

“Anafunga anatoa pasi za mabao unadhani nini tunakihitaji kutoka kwake bado kuna kazi kubwa ipo kwa kila mmoja mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” alisema Kamwe.

MAGAZETI: YANGA YAIMALIZA TP MAZEMBE KIMAFIA…CHAMA AINGIA ANGA ZA SAMATTA KOCHA YANGA AMPIGA CHINI MCHEZAJI MMOJA…KIKOSI CHA KWANZA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply