Habari za Yanga
Habari za michezo

PAMOJA NA YANGA KUINGIA ROBO FAINAL CAF….ALLY KAMWE AANIKA TIMU WANAYOIHOFIA KUKUTANA NAYO…

admin March 27, 2023 8:09 pm

Baada ya kufanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shiriko Afrika, uongozi wa Yanga umeibuka na kutamka kuwa levo ambazo wanazo, wao sio wa kuihofia timu yoyote.

Kauli hiyo imekuja mara baada ya Yanga kuwafunga mabao 2-0 US Monastir ya Tunisia katika mchezo wa tano wa Kundi D kunako Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa juzi Jumapili, Uwanja wa Mkapa, Dar.

Yanga imefuzu hatua hiyo, ikiwa bado ina mchezo mmoja dhidi ya TP Mazembe baada ya kukusanya pointi 10 sawa na US Monastir.

Akizungumza nasi, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema: “Ninaamini baadhi ya timu zitakuwa zimejifunza jinsi ya kuzifunga timu za Waarabu baada ya sisi kuwafunga US Monastir mabao 2-0.

“Kwa levo ambazo tumezifikia Yanga, sisi hatuihofii timu yoyote bali sisi ndio tunahofiwa, hiyo inaonesha ni jinsi gani tuna kikosi bora msimu huu.

“Hivyo Wanayanga waondoe hofu, kwani tofauti na wachezaji bora tuliokuwa nao, pia tuna benchi bora kla ufundi linaoongozwa na Nabi (Nasreddine).”

KISA KIPIGO CHA GOLI 7-0….BEKI HOROYA AENDELEA KUWEWESEKA NA JINA LA CHAMA…AFUNGUKA ALIVYOTESWA… JISAJILI LEO UPATE MPAKA MIZUNGUKO 50 BURE NDANI YA KASINO YA MERIDIANBET…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply