Habari za Yanga
Habari za michezo

MORRISON AIBUKA UPYA YANGA…ALLY KAMWE ATOA KAULI YA KLABU…NKANE NAYE NDANI…

admin March 29, 2023 1:51 pm

Ripoti kutoka kwenye kambi ya Yanga zinasema kuwa kiungo wa pembeni wa klabu hiyo, Bernard Morrison ameshapona kwa asilimia 80 na muda siyo mrefu atarudi kwenye mechi za ligi na kimataifa.

Ripoti hiyo ilitolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, ambaye alisema mambo ni mazuri kwa Morrison na wachezaji kama Denis Nkane ambao walikuwa majeruhi na tayari wameshaanza mazoezi.

“Timu ya wachezaji ambao wamebaki kwenye timu kwa kutoitwa kwenye timu zao za taifa wanaendelea vizuri na mazoezi na wale waliokuwa majeruhi wapo sawa.

“Nkane yeye ameshapona na yupo tayari kucheza mechi ya ushindani na kwa Morrison yeye amepona kwa asilimia 80, nafikiri kwenye mechi zijazo za ligi anaweza kuwa sehemu ya timu,” alisema.

Yanga wanajiandaa na mchezo wao wa mwisho wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe utakaochezwa DR Congo. Baada ya hapo watarudi kujiandaa na Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba na Morrison anaweza akawepo kwenye mechi hiyo.

WAKATI ISHU YA FEI TOTO NA YANGA IKIWA BADO MBICHI…SHAFIIH DAUDA AMPELEKA BACCA AZAM FC… WACHEZAJI SIMBA WAPEWA MASHARTI HAYA…ASIYEWEZA AONDOKE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply