Habari za Simba SC
Habari za michezo

TSHABALALA ‘OUT’ DHIDI YA RAJA….HAWA HAPA MASTAA WENGINE 6 WA SIMBA WATAKAOKOSEKANA..

admin March 30, 2023 11:31 am

Simba itamkosa nahodha msaidizi Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca Jumamosi wiki hii nchini Morocco kutokana na kuwa na kadi mbili za njano.

Kikosi cha Simba kimeanza safari ya Morocco juzi jioni kikiwa na wachezaji 13, huku wengine tisa wakitarajiwa kuungana na wenzao kesho baada ya kukamilisha majukumu ya timu za Taifa.

Licha ya Tshabalala, wachezaji wengine sita watakaokosekana kutokana na sababu mbalimbali ni Mohammed Outtara, Jonas Mkude, Augustine Okrah, Jimyson Mwanuke, Ismail Sawadogo na Mohamed Mussa.

Meneja wa Habari wa Simba, Ahmed Ally ameeleza kuwa mchezo wao dhidi ya Raja Casablanca unataraji kupigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Mohamed V na unatarajai kuanza saa 4 usiku kwa saa za Morocco, ambapo kwa Tanzania itakuwa ni saa 7 usiku.

KOCHA YANGA “MNATAKA KUMUONA MORISSON?…MTAMUONA ATAKAPOFUNGA KAKOLANYA AWAVURUGA MABOSI SIMBA…..SINGIDA BIG STARS ‘WAMTUPIA’ DONGE NONO LA USAJILI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply