Habari za Yanga SC
Habari za Yanga

SAFARI YA YANGA YAINGIA DOSARI…WAKWAMA AIRPORT ZAIDI YA MASAA 12…ISHU NZIMA IKO HIVI

Marce Ben Komba March 31, 2023 8:49 am

SAFARI ya kikosi cha Yanga ikielekea jijini Lubumbashi imeingia dosari baada ya kukwama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere namba tatu kwa masaa 12.

Yanga inakwenda Lubumbashi kumalizana na wapinzani wao TP Mazembe katika mchezo wa mwisho wa Makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Kikosi hicho kiliwasili Uwanja hapo majira ya saa 3:00 kwa safari hiyo ambayo awali ilikuwa ianze saa 5:00 asubuhi ikielekea Lubumbashi kupitia Ndola Zambia.

Hata hivyo muda huo ulipofika walipewa taarifa ya kwamba ndege yao itachelewa na kupangwa kuondoka saa 8:00 mchana lakini pia baadaye ukasogezwa tena mbele na kuambiwa wataondoka saa 11 jioni.

Safari hiyo ikapigwa tena ‘kalenda’ wakiambiwa muda mpya wa kuanza safari hiyo wakitumia Ndege ya Shirika la Tanzania kuwa itakuwa saa 1: 00 usiku lakini mwakapokea tangazo jipya kuwa wataondoka saa 3:00 usiku wakitumia Ndege namba TC 213 sababu ikitajwa kuwa sababu za kiufundi. Wamefika lubumbashi masaa 6 yaliyopita kutoka sasa

MO DEWJI AMTAKA MAYELE SIMBA…GSM ATOA KAULI YA KUTISHA AFRIKA SIMBA YAMUWINDA KIUNGO HUYU HATARI WA KIMATAIFA…GEORGE MPOLE ANYOOSHA MIKONO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply