Home Habari za michezo BAADA YA KUANZA KUPATA NAFASI YANGA….MWAMNYETO AVUNJA UKIMYA…AFUNGUA A-Z ALIYOKUWA AKIPITIA…

BAADA YA KUANZA KUPATA NAFASI YANGA….MWAMNYETO AVUNJA UKIMYA…AFUNGUA A-Z ALIYOKUWA AKIPITIA…

Habari za Yanga
[the_ad id="25893"]

Bakari Mwamnyeto, hakuanza vizuri msimu huu, lakini kwa sasa beki na nahodha huyo wa Yanga yupo moto na mwenyewe amefichua kilichombeba kikosini, huku akichimba mkwara gari limewaka na anazidi kujipanga kuibeba timu hiyo.

Mwamnyeto alipoteza namba kikosini mwanzoni mwa msimu kutokana na kushuka kiwango na nafasi ya beki ya kati kutumika zaidi Dickson Job, Yannick Bangala na Ibrahim Bacca, lakini katika mechi za hivi karibuni amerejea kwenye kiwango chake na kufunika kwenye michuano ya CAF.

Kwa mechi za hivi karibuni katika Ligi Kuu hadi kuanzia katika mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe , Mwamnyeto alipewa nafasi na ameonyesha kiwango kizuri hadi sasa katika mchezo wao uliopita dhidi ya Real Bamako uliochezwa katika uwanja wa Mkapa na Yanga kushinda 2-0 na akizungumza na Mwanaspoti alisema presha alizokuwa nazo awali zimeisha.

Mwamnyeto alisema wakati anakaa benchi au kukosekana uwanjani alikuwa akiumia, lakini aliweza kuhimili presha kwani alijua kabisa katika kazi yoyote ile lazima kuwe na changamoto ndio maana amefaniwa kwa sasa kurudi kwenye ubora wake.

“Ukijua katika kazi kuna changamoto basi kwanza unatakiwa kuzihimili na kujua, maneno yapo tu na huwezi kuyakwepa kabisa maana ukikosea watakusema na ukipatia watakusifia. Kwangu hakukuwa na shida, bali ni upepo kukaa vibaya na kwenye maisha kuna kupanda na kushuka tu,” alisema.

Beki huyo wa zamani wa Coastal Union, alisema wakati wote ambao alikuwa hapati nafasi hajawahi kukata tamaa kabisa kwa sababu alikuwa anajua ipo siku atarudi katika kikosi cha kwanza.

“Ni kujitua tu hakuna kinginine, labda kufuata maelekezo ya kocha na kufanya mazoezi kwa bidii, kwenye maisha yetu sisi au sehemu yoyote ile haupaswi kukata tamaa.”

Akizungumzia upande wa kuwa kwenye kikosi cha raundi ya nne chs kombe la Shirikisho (Caf) alisema anajivunia katika hilo kama mchezaji kwani ni sehemu ya mafanikio.

“Kwangu mimi nasikia furaha sana maana sio mimi bali kila mchezaji ana furaha sana kuingia kwenye kikosi hicho, najivunia sana kwa upande wangu kama mchezaji,” alisema Mwamnyeto na kuongeza; “Tunajua kuna mabao ambayo tumeruhusu lakini kila siku tunafanyia kazi mazoezini kuhakikisha hayajirudii.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here