Home Habari za michezo HII HAPA LALA SALAMA YA SIMBA KIMATAIFA..WAKITAKA KUTOBOA WANAPASWA KUZINGATIA HAYA..

HII HAPA LALA SALAMA YA SIMBA KIMATAIFA..WAKITAKA KUTOBOA WANAPASWA KUZINGATIA HAYA..

Habari za Simba

Upepo unavuma lakini hakuna ajuaye unatokea upande gani na unagotea upande upi. Bado haujaelewa basi fahamu tu kuwa kesho Jumanne itafahamika kuhusu mwendo wa wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ni Simba anbao wana kibarua cha kumenyana na Vipers ya Uganda, Uwanja wa Mkapa ikiwa ni mchezo wa nne baada ya kupasuka mechi mbili ile dhidi ya Horoya ugenini na Raja Casablanca, uwanjani hapo.

Hii ni mechi muhimu kwa timu zote mbili kwa kuwa atakayepata ushindi atakuwa amejitengenezea njia ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa upande wa klabu barani Afrika.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa matumaini kufuzu hatua ya robo fainali yameanza kuonekana.

“Ikiwa tutashinda mchezo wetu dhidi ya Vipers hapo yale matumaini yakufuzu hatua ya robo fainali yatazidi kuwa haikwa kuwa tutakuwa na pointi sita na bado tuna mchezo mmoja mkononi hapa nyumbani.

“Sisi tunapambana na hali zetu kwa sasa na tumechagua hilo huku malengo ikiwa ni kupata matokeo chanya mashabiki wazidi kuwa bega kwa bega nasi inawezekana.

UBUTU WA WASHAMBULIAJI MTEGONI

Mechi tatu za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi siyo Moses Phiri, John Bocco wala Habib Kyombo ambao hata mmoja wao katupia licha ya kupewa nafasi. Hata Jean Baleke naye ngoma ni nzito, hivyo ule ubutu wa safu ya ushambuliaji inaingia kwenye mtego mwingine kuonyesha uwezo wao ndani ya dakika 90 nyumbani.

REKODI KUJENGWA AMA KUBOMOLEWA

Ile rekodi ya Kwa Mkapa hatoki mtu ilibomolewa vipande vipande na ubao uliposoma Simba 0-3 Raja Casablanca. Wakiwa ugenini Raja walisepa na pointi tatu mazima.

NYOTA HAWA WATIBUAJI SENTAM YUNUS
Kwa mabeki wa Simba huyu Yunus siyo mtu mzuri akiwa ni mkali kwenye kuliandama lango awapo uwanjani.

Manula anakumbuka majaribio sitaya Yunus haya kulenga lango lakini yalikuwa na hatari jambo lililofanya mabeki wa Simba kumchezea faulo.

HILALY MUKANDARA
Hapa washambuliaji wa Simba wanakazi ya kubadili mbinu kupita kwa mwamba huyu ambaye hapitiki kirahi si kwenye eneo la ulinzi alipofanikiwa kutimiza majukumu yake kuwazuia Simba zaidi ya mara sita kuwatungua mabao mengi.

ASHARAF MANDELA
Kushoto, kulia unamkuta akifanya yake mzuri kwenye kumwaga krosi ambapo kwenye mchezo uliopita alifanya hivyo zaidi ya mara tano huku pasi zake zikiwa ni elekezi nachonganishi.

Kwenye kuzuia pia ni kikwazo kwakuwa alifanya hivyo zaidi ya mara sita wakiwa nyumbani na anajiamini.

MILTON KARISA
Mwamba mmoja hivi ambaye ana spidi kubwa na aliwakimbiza mabekiwa Simba mchezo ule wa kwanza nchini Uganda bahati mbaya alipata maumivu dakika ya 44 nafasiyake ikachukuliwa na Ibrahim Orit.

Uwezo mkubwa kwenye kupiga krosi ambapo alipiga zaidi ya krosi tatu na mzuri kwenye mikato ya kimyakimya pamoja na mashuti kuelekea lango ambapo alifanya hivyo dakika ya 34.

Ally amesema kuwa hawakutarajia kilichotokea, ilikuwa ni maajabu na matokeo hayo bado hayaaminiki.

“Hakika yale matokeo dhidi ya Raja Casablanca yalitushangaza, ilikuwa ni siku bora kwao na siku mbaya kwetu sasa mchezo wetu dhidi ya Vipers kazi itafanyika kweli kweli.

KOSI LIMESHATUA DAR
Kwa mujibu wa Ally kikosi cha Vipers kutoka Uganda kimetua Bongo jana kwa ajili yamaandalizi ya mwisho yamchezo huo.

Vipers waliingia Bongo wakiwa wametoka kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Simba ambao wanahitaji ushindi kwenye mchezo huo ili kupata pointi tatu.

SOMA NA HII  GAMONDI AFUNGA HESABU ZA USAJILI YANGA......., KUFANYA MAAMUZI MAZITO...