SINGIDA BS YAITETEMESHA YANGA...WAJIHAKIKISHIA USHINDI...WAFIKE KIMATAIFA
Habari za michezo

SINGIDA BS YAITETEMESHA YANGA…WAJIHAKIKISHIA USHINDI…WAFIKE KIMATAIFA

Marce Ben Komba April 19, 2023 10:33 am

Uongozi wa Klabu ya Singida Big Stars umechimba mkwara kuelekea mchezo wa Mzunguuko wa 27 wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao utawakutanisha na Mabingwa watetezi Young Africans mwezi Mei kwenye Uwanja wa Liti mjini Singida.

Singida ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa imebakiza michezo minne kukamilisha msimu huu jambo ambalo wameahidi kufia uwanjani.

Meneja wa Singida Big Stars, Ibrahim Mohammed amesema, wanatafuta nafasi ya kujihakikishia kushiriki michuano ya kimataifa, hivyo wamejipanga kupata ushindi kwenye michezo yote minne iliyosalia.

“Lengo letu kwa sasa ni kumaliza katika nafasi ya tatu ili tupate nafasi ya kushiriki kimataifa msimu ujao, hivyo tayari sisi kama uongozi tumeshazungumza na wachezaji na wameahidi kufanya hivyo.

Njia pekee ya kuhakikisha tunatimiza hilo ni kupata ushindi kwenye michezo yetu yote iliyosalia, hivyo hatutarajii kuiona timu ikija hapa Singida na kutoka na ushindi dhidi yetu,” amesema.

Young Africans itakwenda Singida ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo wa Mzunguuko wa 26 Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba SC kwa kufungwa 2-0, Juzi Jumapili (April 16).

Hata hivyo kabla ya kuelekea mjini Singida, Young Africans itachezamchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

Mchezo wa mkondo wa kwanza utashuhudia Young Africans ikicheza ugenini Nigeria April 23, kasha itarejea jijini Dar es salaam kukipiga katika Uwanja wa Benjamin Mkapa April 30.

ILE MECHI NA SIMBA YAWACOST YANGA…RIVERS HAWAKUWA MBALI  “TUMEGUNDUA HILI SPIKA WA BUNGE AMWAGA MAMILIONI…TIMU HII YAPOKEA MAPENE HAYO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply