MAYELE AMPA SHAVU FEI TOTO CONGO...VIGOGO HAWA WA SOKA KUMSAJILI
Habari za michezo

MAYELE AMPA SHAVU FEI TOTO CONGO…VIGOGO HAWA WA SOKA WANAMPA JEURI

Marce Ben Komba April 20, 2023 7:50 am

Taarifa kutoka ndani ya TP Mazembe ya nchini DR Congo sehemu anayotoka mshambuliaji Fiston Mayele, zinaeleza kuwa uongozi wa timu hiyo upo katika mipango ya kumsajili kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto‘ ambaye bado ana mgogoro na timu hiyo.

Feisal bado anasakata lake na Yanga ambapo mwenyewe ameomba kuondoka ndani ya timu hiyo huku akiwa nje ya dimba kwa zaidi ya miezi 4 sasa.

TP Mazembe hii sio mara yao ya kwanza kumtaka mchezaji huyo ambapo taarifa zinadai kwa sasa timu hiyo imerudi tena na sasa iko siriaz kumtaka kiungo huyo.

Chanzo chetu cha ndani kutoka TP Mazembe kimeliambia Championi Jumatano juu ya timu hiyo kuwa katika mipango ya kumsajili Feisal kwa gharama yoyote hiyo ni kutokana na kuhitaji kukiimarisha kikosi chao na kurudisha makali yake kama alivyokusudia Moise Katumbi ambaye ni bosi wa timu hiyo.

“Bosi Katumbi yupo katika mipango ya kuirudisha TP Mazembe katika ubora ule wa awali ambao watu wameuzoea, amechoshwa na kiwango kibovu cha timu na ameahidi kufanya usajili wa maana.

“Mmoja kati ya wachezaji ambao wameorodheshwa kwenye usajili mkubwa ni Feisal Salum kutoka Yanga, amekuwa kipenzi cha tajiri ambaye ameweka wazi kuwa tayari kumpata kwa gharama yoyote.

“Nadhani kupitia dirisha kubwa la usajili kila kitu kitakuwa wazi lakini lazima nikuambie kuwa Feisal yupo katika mipango ya TP Mazembe,” kilisema chanzo hicho cha kuaminika.

Feisal alipotafutwa kwa ajili kujibu jambo hilo aligoma kuzungumza chochote.

CAF WAIBEBA SIMBA SC MBELE YA WYDAD……WAPEWA REFA WA USHINDI…BALAA LAKE HILI HAPA… SIMBA YAKIMBILIA CAF MECHI NA WYDAD…VAR ITATUMIKA…MANULA,KANOUTE OUT

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply