Sadio Mane
Habari za michezo

KISA KUMTANDIKA SANE NGUMI ZA USO…MANE APIGWA FAINI YA MIL 724….HUENDA AKAPIGWA BEI MAZIMA…

admin April 20, 2023 4:10 pm

Baada ya Sadio Mane kumpiga mchezaji mwenzake wa bayern Munich, Leroy Sane wiki iliyopita nyota huyo amepigwa faini ya pauni 250,000, (Sh.724,445,000).

Pia inatajwa kuwa staa huyo raia wa Senegal yupo kwenye hesabu za kuuzwa mwishoni mwa msimu huu.

Mane alimchapa ngumi ya mdomo Sane kwenye chumba cha kubadilishia nguo wiki iliyopita kwa madai kuwa Sane alimkejeli kwa lugha na vitendo vya kibaguzi baada ya mchezo dhidi ya Manchester City.

Sane alionekana akiwa amevimba mdomo wakati Bayern Munich walipoivaa Hoffenheim wikiendi iliyopita na Mane hakuwepo kwenye mchezo huo wa Bundesliga.

Mane amesimamishwa kwa kitendo hicho huku akikatwa mshahara wake wa pauni milioni 17, (sh.49.2) kwa mwaka. Hii ni faini kubwa kwa Bayern Munich kutolewa katika historia yao.

KOCHA MAARUFU AFRIKA AIPELEKA YANGA SC NUSU FAINAL CAF…AWAPA MBINU ZA KUPITA… BAADA YA KUSAIDI DILI JIPYA YANGA SC…JOB AFUNGUKA A-Z SABABU ZA KUITOSA SIMBA SC…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply