Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA WANIGERIA….MCHAMBUZI BONGO AWAKUMBUSHA YANGA SC MAMBO YA SIMBA..

KUELEKEA MECHI NA WANIGERIA….MCHAMBUZI BONGO AWAKUMBUSHA YANGA SC MAMBO YA SIMBA..

Habari za Simba SC

Mchambuzi maarufu wa masuala ya soka nchini, Ramadhani Mbwaduke amesema kuwa Klabu ya Yanga SC wanayo nafasi ya kushinda katika mchezo wao wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rivers United.

Mbwaduke amesema kuwa hayo yanawezekana iwapo kocha wa Yanga SC na benchi lake la ufundi watayafanyia kazi mapungufu ya mchezo wao dhidi ya watani zao Simba uliopigwa wikiendi iliyopita na Yanga kukubali kichapo cha bao 2-0.

Aidha, Mbwaduke amesema kuwa mfumo wanaotumia Rivers ni kama walivyocheza Simba kipindi cha kwanza cha mchezo wao na Yanga SC wakianza kukabia juu hivyo Yanga wanayo nafasi ya kutafuta mbinu ya kuwafungua wapinzani wao ili kufanikisha mipango yao ya kupata matokeo.

“Mechi ya dabi imewapa somo sana Yanga, nina uhakika benchi la ufundi la yanga limejaa watu mafundi wa kujua kasoro ipo wapi, na waboreshe wapi. Simba imewapa shoo Yanga ambayo inafanana na Rivers United.

“Cheza ya Rivers United ni kama Simba alivyocheza kipindi cha kwanza dhidi ya Yanga. Mechi ya Rivers dhidi ya ASEC Mimosas, Rivers alishinda 3-0 na walicheza kama Simba.

“ASEC, Yanga na Monastri ndio timu zilikuwa na matokeo mazuri kuliko zote hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho wote wana alama 13 wwmepishana tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, ukiwapanga Yanga ndiyo anakuwa juu yao anaongoza kwa matokeo mazuri.

“Mechi dhidi ya ASEC, Rivers walikuwa anafanya high pressing wakikabia kutoka juu, ndiyo wnaoongoza kwa kucheza madhambi kwa mujibu wa rekodi za CAF, ni kama wanavyofanya Chama, Kibu, Sakho na Saido kwa Simba.

“Rivers wanaisoma Yanga, wanajua ni wazuri wa kumiliki mpira kama ASEC, watakachokifanya naamini ni kama alichokifanya Simba mechi ya dabi. Kwa hiyo Yanga wachukue picha ya Simba kipindi cha kwanza, ndiyo waifanye kama Rivers United watakavyokuja, ndipo watafute mbinu za kuweza kupenyeza mipira badala ya kuanzia kwa mabeki, kwa sababu wata-block zile njia zao.

“Naamini mechi ya dabi wataitumia vizuri Yanga kwa sababu pia wanakwenda kukutana na timuambayo wapo kwenye nafasi moja ya ubora wa viwango vya CAF, yaani wote wapo nafasi ya 28 barani Afrika wote wakiwa na pointi 10,” amesema Mbwaduke.

SOMA NA HII  KUHUSU KUFUNGA SANA MAGOLI .....MUDATHIR HUYU HAPA....AANIKA KILICHONYUMA YAKE...