Home Habari za michezo HIZI HAPA SIKU 109 ZA MBRAZILI NDANI YA SIMBA SC….WALIOSEMA HAWEZI WAKIMBIA...
- Habari za michezo
- Habari za Simba
- Habari za Simba Leo
- Michezo
- Michezo Bongo
- Michezo Soka la Bongo
- news
- Simba SC
Wakati anatua Simba SC aliikuta tayari imeshatinga hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, akipokea kazi nzuri ya aliyekuwa kocha wa muda, Juma Mgunda ambaye sasa ni msaidizi wake wa kwanza ndani ya kikosi hicho.
Kama kuna tukio ambalo lilitishia maisha ya Robertinho Simba ni Januari 18,2023 Simba ikicheza nyumbani dhidi ya Mbeya City na ndani ya dakika 30 akamtoa kiungo fundi Clatous Chama na kumuingiza winga Pape Sakho.
Takribani misimu mitatu Simba ilikuwa haijawafunga watani wao wa jadi Yanga, mara ya mwisho wekundu hao kushinda ilikuwa mwaka 2019.
Kama hufahamu ni kwamba Robertinho ambaye ni winga wa zamani wa Brazil ameiongoza Simba katika jumla ya mechi 14 za mashindano yote na katika hizo 7 ni za ligi kuu bara na hajawahi kupoteza mechi yoyote.
Simba chini ya Robertinho inaendelea kupigania heshima ya klabu hiyo licha ya changamoto za ubora wa wachezaji ambazo zilikuwa zinaonekana kabla, Robertinho ameifanya timu hiyo kuruhusu mabao manne tu kwenye ligi lakini ikifunga 15.
Kimahesabu huwezi kumuondoa Simba katika mataji matatu, ikiwa bado inaikimbiza Yanga ambao wanaongoza msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 5 baada ya kushinda wikiendi iliyopita Robertinho alipunguza pengo hilo kwa alama tatu kutoka 8 za awali.